Rais wa Brazil Dilma Rousseff amechaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo.
Matokero rasmi ya uchaguzi huo yanaonesha Bi Rousseff ameshinda kwa Asilimia tatu ya kura katika uchaguzi uliojaa ushindani mkali dhidi ya mpinzani wake, mwanasiasa mwenye mrengo wa kati kulia Aecio Neves, ambaye tayari amekubali kushindwa.
Akiwashukuru wapiga kura wake, Dilma Rousseff amesema anataka kuwa Rais bora zaidi na kipaumbele kikuu katika awamu yake ya pili ya uongozi itakuwa ni kufanya mageuzi ya kisiasa.
Mwandishi wa BBC nchini Brazil amesema wapiga kura wameamua kuendelea kumchagua, Bi Rousseff wakiunga mkono mfumo na chama ambacho kimeukuza uchumi wa nchi hiyo na mipango mingi kuhusiana na ustawi wa jamii hiyo, ambavyo vimewatoa katika umasikini uliokithiri.
BBC
0 comments:
Post a Comment