muonekano wa jiji la Dar es salaam
Kama ulifika Dar es Salaam miaka mitano iliyopita, ukija sasa bila shaka utashtushwa na ujenzi wa kasi wa majengo marefu na ya kisasa katikati ya jiji hilo.
Majengo pacha ya PSPF Business Towers, Golden Jubilee Towers, Uhuru Heights, Mawasiliano Towers na LAPF Millenium Towers ni miongoni mwa majengo yanayovutia na ni kielelezo kinachoonyesha kasi ya maendeleo katika sekta ya ujenzi.
Ukweli ni kwamba, kila kona ya jiji majengo mazuri zaidi yanaibuka huku yale ya zamani yenye mvuto wa kihistoria yakivunjwa. Mifuko ya hifadhi ya jamii inaongoza kuwa na majengo mengi ya kisasa yenye kuvutia.
Wakati miaka miwili iliyopita majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yalikuwa yakiongoza kwa uzuri, kwa sasa ‘siyo habari tena ya mjini’.
Nyumba kukuu zilizokuwapo katika mitaa ya Kariakoo zinazidi kutokomea na sasa eneo hilo limetawaliwa na majengo marefu yenye hoteli na maduka ya kisasa.
Maeneo mengi ya katikati ya jiji ambayo zamani yalikuwa na miti japo kidogo, bustani na maeneo ya wazi, sasa yamejengwa majengo marefu ya biashara, makazi na maegesho ya magari ya ghorofa.
Wakati baadhi ya watu wakiendelea kuduwazwa na uzuri wa majengo hayo, hali ya mipango miji si shwari katika maeneo yapembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.
Hivi sasa kuna ongezeko kubwa la ujenzi wa makazi holela katika maeneo ya Tandika, Kisukuru, Mbagala, Kimara Bonyokwa, Manzese na kwingineko.
Karakana za magari na viwanda bubu vinazidi kuongezeka hadi kwenye makazi ya watu huku ‘wajasiriamali’ wadogo nao wakiendelea kumomonyoa kingo za mito kwa kuchimba mchanga wa biashara katika baadhi ya maeneo inakopita mito. Matukio hayo kwa hakika yanatia dosari mwonekano mpya wa Jiji la Dar es Salaam.
Utunzaji wa mazingira unaonekana bayana kutoendana na kasi ya maendeleo ya jiji hilo na miji mingine nchini, kitendo ambacho wataalamu wa mazingira na maendeleo ya makazi wanaona ni hatari kwa mustakabali wa Taifa.
Wanasema kasi ya maendeleo inatakiwa iendane na utunzaji wa mazingira ili kuifanya miji kuwa mizuri zaidi.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Richard Muyungi takriban asilimia nane ya ardhi ya Dar es Salaam, watu 140,000 na mali zenye thamani ya Sh280.5 bilioni, viko hatarini kuathiriwa na mafuriko.

No comments:
Post a Comment