Majaji wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ya ICC iliyoko The Hague,Uholanzi wamesema mke wa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Simonne Gbagbo anapaswa kukabidhiwa kwa mahakama hiyo kufunguliwa mashitaka dhidi yake.
Simonne,mke wa Laurent Gbagbo anatuhumiwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu.
&nbs
Serikali ya Ivory Coast imekataa kumsalimisha kwa mahakama ya ICC ikisema itamshitaki kwa mauaji ya halaiki katika mahakama za nchini humo.
Gbagbo mwenyewe na mshirika wake Charles Ble Goude wanazuiwa katika mahakama ya ICC kwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Watatu hao wanatuhumiwa kwa kulitumbukiza taifa la Ivory Coast kwa ghasia baada ya uchaguzi mwaka 2010 ambapo kiasi ya watu 3,000 waliuawa baada ya Gbagbo kukataa kuondoka madarakani baada ya kushindwa na Alassane Qattara.
No comments:
Post a Comment