Pages

2014-12-04

KAMATI YA KUSIMAMIA TUZO ZA TASWA YATOA ORODHA YA WANAMICHEZO WANAOWANIA TUZO HIZO


 
KAMATI ya Kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kupitia majina ya wanamichezo waliopendekezwa kuwania tuzo hizo.

Usiku wa Tuzo utafanyika Desemba 12 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee (VIP), Dar es Salaam, ambapo wanamichezo mbalimbali waliofanya vizuri kati ya Juni 2013 hadi Juni 2014 watakabidhiwa tuzo zao.

Ni imani yetu kwamba zaidi ya wanamichezo 40 watakabidhiwa tuzo zao siku hiyo, ambapo kamati imejiridhisha kwamba wanaowania tuzo hiyo wanastahili kulingana na mapendekezo ya vyama vya michezo kupitia Kamati zao za Ufundi.

Mshindi wa kila tuzo ataingia katika mchakato wa kumpata Mwanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2013/2014, ambapo pia siku hiyo ya sherehe za tuzo itatangazwa zawadi ya Tuzo ya Heshima kwa yule ambaye itaonekana alikuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya kimichezo hapa nchini.
 
 Tuzo hizo ni kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014.
ORODHA KAMILI YA WANAOWANIA TUZO ZA TASWA 2013/2014
 

 Michuzi

No comments:

Post a Comment