Watu wawili wamekufa na wanane kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Mwada na kuhusisha gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Magara kuelekea Magugu na Babati.
Aidha, ajali hiyo ilizua mvutano mkubwa baada ya wahudumu na maofisa wa kituo cha afya kugoma kupokea majeruhi wakidai wapewe fedha kwanza.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Deus Nsimeki, alitaja gari hilo kuwa ni T .728 CLV na kuwa dereva wake, Kazumba Musa aliyekimbia baada ya ajali hiyo, anatafutwa.
Alisema gari hilo lililokuwa na abiria kumi lilipinduka kisha kugonga mti baada na kuvutwa na mchanga.

Waliokufa ni Godlack Loshiye (25) na mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Angela.
Waliojeruhiwa ni Niko Demu, Maganga Sele, Rasuli Abdallah, Abdallah Mohamed, Edward Machel, Yuda Sanga, Lucia Francis, Paskalina Jovita, Saumu Hamisi, Anna Bernard na Tekla Leonard.
Katika tukio lingine, wauguzi na madaktari katika Kituo cha Afya Magugu walikataa kupokea miili ya marehemu na majeruhi wakidai kupatiwa Sh. 50,000 kwanza.
Hali hiyo ilizuwa tafrani kubwa kati yao na ndugu na jamaa wa marehemu pamoja na majeruhi, hali iliyoulazimisha uongozi wa Wilaya ya Babati Vijijini akiwamo Mkurugenzi Mtendaji kufika katika kituo cha afya.
Viongozi hao walikwenda kituoni baada ya kupigiwa simu na wananchi waliofika kutambua miili ya marehemu.
Mmoja wa wahudumu wa kituo hicho alidai mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Babati, Dominick Kweka, kuwa hawezi kushika damu ya mtu hadi apatiwe kitita walichokitaka Hali hiyo ilimkasirisha Kweka aliyefuatana na madaktari wa wilaya na kuamuru polisi kuwakamata wote waliyokataa kuwapokea majeruhi na kudai rushwa.
Pia aliamuru kukamatwa kwa nesi aliyekuwa amefuatana na wagonjwa wengine kwenda hosptali ya Dareda akamatwe baada ya kubainka kuwa aliwatelekeza wagonjwa baada ya kufika Babati mjini.
No comments:
Post a Comment