Pages

2014-12-11

SHOCKING: DAKTARI FEKI AKAMATWA KATIKA TAASISI YA MIFUPA MUHIMBILI ( MOI )



Daktari feki aitwaye Dismas Macha amekamatwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) akiwa amevaa sare za kazi kama Daktari ambapo hii inakuwa mara ya pili kukamatwa akiwa anachangisha rambirambi kwa Madaktari akidai kuwa amefiwa.


Anaye daiwa kuwa Daktari feki, akiwa chini ya ulinzi Dar es Salaam jana, baada ya kuingia katika Taasisi ya Mifupa (MOI) akiwa amevalia nguo ya kazi na akiwa na kitambulisho cha kazi na kujifanya yeye ni Daktari wa Taasisi hiyo. 
Baada ya kukamatwa na askari alikutwa na vitu mbalimbali kama vile nyaraka za Serikali.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo ya MOI, Dk Othman Wanin Kiloloma amesema.

No comments:

Post a Comment