

WENGI WANATESEKA
Wanaume wengi waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao, wamekiri kwamba wanazichukia ndoa zao na wanawachukia wake zao kwa sababu ya kutumia tendo la ndoa kama silaha kila wanapogombana.
“Mimi mpaka imefika mahali nimeamua kuwa naenda kununua machangudoa kwa sababu mke wangu hanipi haki yangu ya ndoa. Ukimuudhi kidogo anakaa hata miezi miwili hana habari na wewe,” hiyo ni sms ya msomaji wangu aliyeomba hifadhi ya jina lake.Wengi wakaendelea kulalamika kwamba kama wanawake hawataacha mchezo huu, daima wataendelea kuchepuka ili kutafuta furaha nje ya ndoa.
MAANA IMEBADILISHWA
Wanawake watu wazima waliotoa maoni yao kama nilivyowaomba, wamekiri kwamba suala la mwanamke kutumia tendo la ndoa kama silaha ya kumnyoosha mume pale anapokosea, haijaanza jana wala juzi. Ipo kwa karne nyingi zilizopita ingawa kizazi cha sasa kimeibadilisha maana nzima ya kitendo hicho.
WAKONGWE WANASEMAJE?
“Enzi zetu wakati tukiwa bado wabichi, mumeo akikuudhi leo basi usiku ‘unamlaza njaa’, akiamka asubuhi mwenyewe anaanza kukubembeleza. Kama kulikuwa na tatizo mnalimaliza, akirudi jioni kakuletea zawadi basi unafurahi maisha yanaendelea lakini ilikuwa haiwezi kuzidi siku moja.

KITU MUHIMU CHA KUJIFUNZA
Kwa kuwa lengo letu ni kuelimishana na kunusuru ndoa nyingi zaidi kuendelea kuvunjika kwa sababu ya wanandoa kunyimana haki zao, ni muhimu kila mmoja akimaliza kusoma mada hii, awe amejifunza kitu ndani ya kichwa chake.
Ugomvi upo na haukwepeki ndani ya ndoa lakini ni makosa makubwa kumnyima mwenzi wako haki yake eti kwa sababu amekuudhi. Wanandoa wanashauriwa, kama kuna ugomvi, kila mmoja atimize wajibu wake kwanza.Kwamba hata kama amekuudhi, mpe kwanza haki yake kisha akishafurahi, zungumza naye kwa upole na mueleze kile ambacho kimekukasirisha.
WANAWAKE CHUKUENI HII!
Wanaume wengi wamekiri kwamba wao ni dhaifu sana linapokuja suala la tendo la ndoa kwa wake zao. Kwamba kama mke anataka kutimiziwa jambo lolote analolitaka, hata liwe kubwa kiasi gani, muda mzuri wa kuzungumza na
mumewe, ni baada tu ya kumaliza kumpa haki yake ya ndoa.
Kama unataka pesa ya saluni, pesa za Vicoba, nguo mpya, kama unataka ufunguliwe biashara au chochote, muda mzuri wa kuzungumza na mwenzi wako, ni pale ukishamaliza kumpa haki yake ya ndoa kikamilifu. Wanaofanya hivi,
wanafanikiwa ila wanaofanya kinyume chake, matokeo yake huwa ni mume kutafuta mchepuko au kutengana kabisa.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.
No comments:
Post a Comment