KAMPUNI ya mtandao wa simu ya Airtel imezindua huduma mpya ya vifurushi vya muda wa maongezi, mtandao na meseji unaokwenda kwa jina la ‘Airtel Yatosha Zaidi’. Huduma hii ina unafuu zaidi ya huduma ya mwanzo iliyotambulika kama ‘Airtel Yatosha’.
Wakizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Mlimani City, Dar, Mkurugenzi wa Masoko Levi Nyakundi na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano, wa Airtel, walisema wateja wao watazawadiwa gari aina ya Toyota IST itakayotolewa kila siku kwa mshindi atakayepatikana baada ya droo ya huduma hiyo kuchezeshwa.
Wakifafanua zaidi kuhusu zawadi hiyo, wakurugenzi hao walisema kwa kupiga *149*99# kununua Airtel Money au kwa kununua vocha za Airtel Yatosha zilizopo kwenye maduka yote nchini, mteja wa Airtel anaweza kujiunga na vifurushi vya ‘Yatosha Zaidi’ na kuweza kuingia katika droo itakayomwezesha kushinda gari hilo. (HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL)
No comments:
Post a Comment