Saikolojia ya kawaida inatufundisha kwamba ukiona mtu anaandamwa kwa kiwango kikubwa, wakati mwingine ujue ni kwa sababu amegeuka tishio kwa uhai, vyeo na madaraka ya wasiompenda.
Yesu Kristo aliandamwa na uongozi wa Kiyahudi siyo kwa sababu alikuwa gaidi au jambazi, bali kwa sababu alikuwa ni tishio kwa mamlaka na vyeo vyao.
Sitaki kumlinganisha Dk Slaa na Yesu, lakini kama mwanadamu mwenzetu kuna yanayofanana na watu wengine duniani waliofanyiwa, hila kama hizo kwa sababu tu walikuwa tishio kwa watawala.
Dk Slaa kwa sasa siyo padri kama wanasiasa wengi wanavyodanganya umma wa Watanzania kwa sababu aliomba kibali cha kuondolewa mamlaka ya kipadri na alikubaliwa.
Kuendelea kumwita padri ni porojo za kisiasa na alama wazi ya hofu ya wapinzani wake kuelekea uchaguzi ujao na kuwapotosha wananchi wasiojua nini kinaendelea katika nchi yetu.
Ni dhahiri Dk Slaa kwa sasa ni mwiba kwa CCM na vyama vyenye mrengo wa CCM vinavyoamini katika siasa zisizo na faida. Kama kiongozi wa chama cha upinzani (Chadema) Dk Slaa ana mvuto wa pekee kwa Watanzania bila kujali dini, itikadi, kabila, vyeo wala tabaka la watu.
Dk Slaa amejizolea sifa nyingi katika utendaji wake pamoja na kurushiwa madongo mengi kwa lengo la kumchafua, lakini mbinu zote chafu zimeshindikana.
Waswahili hutumia neno ‘jembe’ wakimaanisha mtu makini na mtendaji na ndilo jina analositahili Dk Slaa, ni mjenga hoja mzuri.
Mtu wa namna hii hata kama utamfanyia fitina, chuki, mizengwe, hujuma ni kama kupoteza muda tu kwa sababu anajifahamu. Kwa mantiki hii, Dk Slaa ni kiongozi mwenye msimamo thabiti na anatetea kile anachokijua kwa nguvu na uwezo wake wote.
DK Slaa aliwahi kudai kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2010, aliporwa ushindi. Kulikuwa na madai kuwa baadhi ya viongozi wa dini walikwenda kumwona ili kumtuliza asiitishe maandamano ya kudai ushindi kama alivyofanya Raila Odinga nchini Kenya mwaka 2007.
DK Slaa aliwahi kudai kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2010, aliporwa ushindi. Kulikuwa na madai kuwa baadhi ya viongozi wa dini walikwenda kumwona ili kumtuliza asiitishe maandamano ya kudai ushindi kama alivyofanya Raila Odinga nchini Kenya mwaka 2007.
Swali, kwa nini Dk Slaa alirudia tamko hilo mbele ya wageni mbalimbali wakiwa mabalozi wa nchi za nje? Alitaka kufikisha ujumbe gani? Watu makini hawakurupuki bali wanapangilia mambo yao.
Kama ni sifa za uongozi, basi Dk Slaa hababaishi. Ni kiongozi mwenye muono, yaani ile hali ya kuweza kuona anakwenda wapi na wengine kumfuata.
Tanzania ya leo imepoteza mwelekeo kiasi cha kulinganisha na meli isiyo na nahodha.
Mwananchi.
No comments:
Post a Comment