…Maamuzi magumu kutolewa kesho Februari 26
LISAA limoja lililopita Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge amepandishwa kizimbani katika kikaango cha kukiuka maadili ya viongozi wa umma, chini ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Baraza la Maadili lililoketi, jijini Dar es Saalam asubuhi ya leo.
Katika shauri linalomkabili Chenge ni dhidi ya kukiuka vifungo hivyo vya sharia ya maadili ya viongozi wa umma, ambapo ilielezwa kuwa, Miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ya ukiukwaji wa sharia ya maadili ya viongozi wa umma, ni pamoja na alipokuwa Mtumishi mkuu wa serikali kwa wadhifa wa mwanasheria Mkuu wa Serikali AG, alipitisha mikataba mbaalimbali dhidi ya IPTL, na baadae alipostaafu nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu alikuwa miongoni mwa Washahuri wakuu wa kampuni ya V.I.P Engineer.
Ambapo ilielezwa kuwa, Chenge hakuwahi kueleza tume hiyo ya Maadili kama ana madai ama ana hisa na kampuni hiyo ya V.I.P ambayo iliingia ubia na IPTL Katika uuzwaji wa hisa hali ambayo moja kwa moja ilipelekea kukiuka vifungu vya sharia.

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge akishuka kizimbani baada ya kikaango.
Hata hivyo, Chenge aliweza kujitetea ambapo aliwasilisha oda maalum ya utetezi wake dhidi ya madai anayodaiwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili wa Baraza hilo anayeshughulikia mashahuri hayo Mhe Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi alisema wataenda kukaa na kupitia oda hiyo ya Chenge na kisha watatoa maamuzi siku ya Februari 26 mwaka huu yaani , (kesho) Alhamisi.
“Tunaenda kupitia vielelezo vyote na maamuzi yatatolewa Februari 26.” Alisema Balozi Msumi.
Hata hivyo baada ya kuahirishwa kwa baraza hilo ambalo litaendelea tena kesho, Chenge alifuatwa na wandishi wa habari ambapo alikataa kata kata kuongea nao huku akiwaambia waende kuandika wanavyo jua wao.

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge akichukua mkoba wake.
“Mnataka nini. Nyie nendeni mukaandike munavyojua … nendeni mkaandike sasa. Siwezi ongea chochote” alikuwa akitamka Chenge huku akitoka kwenye ukumbi wa Karimjee yanakofanyika mashitaka ya baraza hilo la Maadili.
Baraza hilo la Maadili bado kesho litaendelea tena na shauri hilo la Chenge pamoja na viongozi wengine wa umma. Mtandao huu utaendelea kukupatia Exclusive za kila kitu kinachoendelea juu ya baraza hili.. endelea kufuatilia sasa…
No comments:
Post a Comment