
FAMILIA ya mzee Wilson Lyimo, mkazi wa maeneo ya Sinza-Makaburini, jijini Dar, imejikuta ikilala nje kwa wiki kadhaa baada ya kuvunjiwa nyumba yao usiku wa manane na watu wanaodaiwa kuwa ni mabaunsa wapatao 60.

Vitu vikiwa nje baada ya nyumba kuvunjwa.
Mabaunsa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo usiku wa kuamkia Februari 24, mwaka huu wakati wanafamilia hao pamoja na wapangaji wawili wakiwa wamelala ndani ya nyumba hiyo.
Chanzo makini kimeeleza kuwa, mabaunsa hao walipofika kwenye nyumba hiyo, waliamuru watu wote waliokuwa ndani watoke nje wakidai wamepewa maagizo ya kuvunja nyumba hiyo na jamaa mmoja (jina tunalihifadhi kwa sasa).
Mabaunsa hao walianza kubomoa kuta za nyumba hiyo bila kujali watoto na wapangaji kama wametoka nje au la ambapo hali hiyo ilisababisha usumbufu na upotevu wa baadhi ya vitu ambavyo thamani yake haikupatikana mara moja.


Kwa mujibu wa mtoto wa kwanza wa familia hiyo, Edwin Lyimo, baba yake anamiliki eneo hilo kihalali tangu mwaka 1977 kwa namba ya kiwanja Block C Namba 68, Namba ya Hati 21818 yenye jina la usajili, Wilson Fataeli Lyimo.
Edwin aliendelea kufunguka kuwa, awali familia hiyo ilikuwa na mgogoro wa muda mrefu na jamaa aliyetajwa na mabaunsa hao kuhusu kiwanja na nyumba hiyo hadi kufikishana Mahakama ya Ardhi lakini ghafla wameshangaa kuona mabaunsa hao wamekuja kuvunja nyumba hiyo.

Jitihada za kumpata jamaa aliyetajwa na mabaunsa hao ili aweze kuzungumzia sakata hilo hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kutopatikana hewani, jitihada
No comments:
Post a Comment