Wachezaji watano Wa klabu ya Kano Pillars wamepigwa risasi na mtu mwenye silaha wakati klabu hiyo ilipokuwa ikisafiri kwa basi kuelekea jimboni Owerri kuanza msimu mpya wa ligi kuu nchini Nigeria.
Wachezaji watano waliojeruhiwa kwa risasi ni Gambo, Ogbonaya, Eneji Otekpa, Murtala Adamu, na Moses Ekpai.
Washambuliaji hao wamewapora simu za mkononi na vitu vingine vya thamani.
Mechi iliyokuwa ifanyike kesho Jumamosi imeahirishwa kwa muda usiojulikana.
Basi hilo lilikuwa limebeba watu 25, wakiwemo wachezaji 18.
Wachezaji hao waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Likoja.
Timu hiyo ilikuwa ikijiandaa kuanza kutetea taji la ligi kuu ya Nigeria baada ya kuanza msimu kwa ushindi dhidi ya Al Malakia katika ligi ya mabingwa ya Afrika katika raundi ya kwanza wiki iliopita
No comments:
Post a Comment