Pages

2015-03-09

Ina sikitisha sanaaaaa: Mtoto mwingine Albino akatwa mkono


Watoto Albino wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili na kuuawa Tanzania

Matukio ya ukatili dhidi ya albino yanaendelea kuwa tishio nchini Tanzania baada ya mtoto wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono

Shambulio hilop jipya limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Mtoto huyo kiume Baraka Cosmas alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto huyo anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.


Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.

No comments:

Post a Comment