Pages

2015-03-07

SNURA AFUNGUKIA UKIMYA WAKE


Msanii wa muziki wa mduara, Snura Mushi 'Snura' akiwa katika pozi.



Mtangazaji wa Global TV, Mourad Alpha (kushoto) akifanya mahojiano na Snura. 


Snura akiwa katika pozi na mtangazaji wa Global TV Online, Mourad Alpha. 



Snura 'Mama Majanga ' akijiachia baada ya mahojiano na Global TV. MKALI wa miondoko ya mduara, Snura Mushi 'Snura' leo alitinga katika ofisi za Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV kupitia kipindi cha Exlusive.Snura alifunguka mengi kuhusiana na ukimya wake ambapo alikiri kuwa mimba ilimuweka pembeni kwa muda lakini kwa sasa amerudi upya na wimbo mpya wa Hawashi.

"Ilikuwa ni ngumu kujitokeza hadharani na kusema kuwa nina mtoto. Nilifanya siri kubwa sana na hata majirani zangu tu hawakuweza kujua kama nina ujauzito kwani nilikuwa mtu wa kushinda na baibui hata pale nilipohitajika kwenda kliniki nilikuwa nikijifunika baibui na nikifika hospitali najifunua," alisema Snura.

Snura ameongea mengi mno kuhusiana na maisha yake na kusema amerudi mara mbili ya zamani kwani wimbo wake mpya umezalisha staili ya aina yake aliyoipa jina la Panya Road.

No comments:

Post a Comment