Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge, akitoa maelezo yake mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma lililokuwa likisikiliza shauri lake hivi karibuni.
Ofisa wa TRA aliwekewa Sh80.9 milioni na mmiliki wa VIP Engeneering and Marketing ambayo ni mteja wa mwajiri wake.
Hadi sasa watu wanne wamekwamisha mashauri yao kusikilizwa na sekretarieti kwa kukimbilia Mahakama Kuu.
Dar es Salaam. Staili ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ya kukwamisha Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kujadili watu wanaohusishwa na fedha zilizochotwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, imezidi kunoga.
Baada ya viongozi watatu kufanikiwa kuchelewesha sekretarieti hiyo kujadili mashauri yao, wakiongozwa na Chenge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, jana Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Loicy Appollo aliomba aende Mahakama Kuu kuomba tafsiri ya zuio la Mahakama kwa vyombo vya Serikali kujadili masuala ya escrow hadi hapo kesi iliyopo Mahakama itakapotolewa uamuzi.

Mtumishi huyo wa TRA aliwekewa Sh80.8 milioni kwenye akaunti yake, fedha ambazo zinahusishwa na Sh306 bilioni zilizotolewa kwenye akaunti hiyo na baadaye kugawanywa kwa watu mbalimbali, wengi wao wakiwa na mawaziri, wabunge na maofisa waandamizi wa Serikali na taasisi zake.
Appollo alisomewa mashtaka na mwanasheria wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mwanaarabu Tale, lakini alikana na baadaye wakili wake, Wilson Ugunde alitoa hoja kwamba Novemba 20 mwaka jana Mahakama Kuu ilizuia suala la Akaunti ya Tegeta Escrow lisijadiliwe na chombo chochote na kwamba anaomba awasilishe maombi ili mahakama itoe tafsiri.
Kama ilivyokuwa kwa watuhumiwa wengine watatu wanaodaiwa kukiuka maadili, mwenyekiti wa Sekretarieti hiyo, Jaji Hamisi Msumi alikubali ombi lake na sasa shauri lake litajadiliwa baada ya mahakama kutoa tafsiri ya zuio lake.
Walioikwepa Sekretarieti
Staili kama hiyo ilianza kutumiwa Chenge ambaye alifikishwa mbele ya Sekretarieti hiyo akikabiliwa na mashtaka ya kupokea Sh1.6 bilioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engineering and Marketing Ltd, James Rugemalira.
Chenge alipofikishwa mbele ya baraza hilo, alisema kuna amri ya Mahakama Kuu ya kuzuia vyombo mbalimbali kujadili suala hilo hadi litakapotolewa uamuzi. Baraza hilo liliahirisha shauri hilo na siku ya pili Jaji Msumi alisema zuio hilo haliihusu Sekretarieti yake na kutaka shauri liendelee kusikilizwa.
Baada ya kuona hayo, Chenge aliomba aende Mahakama Kuu ili kupata tafsiri na Jaji Msumi alimruhusu na hivyo Sekretarieti kushindwa kujadili shauri hilo.
Wengine waliolikwepa baraza kwa staili hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita), Philip Saiboko ambaye alipokea Sh40.4 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engineering and Marketing Ltd.
Mwingine ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma anayekabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh423.4 milioni kutoka Kampuni ya VIP Mabibo Wines and Spirit.
Mujunangoma mbali ya kutumia staili ya zuio la Mahakama Kuu, pia kupitia Wakili wake Jamhuri Johnson alisema ana kesi namba 11 katika Mahakama ya Kisutu inayohusu Akaunti na Tegeta Escrow.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment