Moshi. Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi limesema tatizo la vijana wengi kujiingiza katika ulevi na uasherati ni kutokana na matumizi mabaya ya utandawazi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu wa jimbo hilo, Isaac Amani katika ibada takatifu ya kuwaombea wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Amedeus , iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, ili waweze kubarikiwa katika mitihani ya kidato cha nne inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Novemba 3 mwaka huu.
“Uashereti kwa sasa umekuwa ni fasheni kwa vijana na hata mtu ambaye hafanyi mambo hayo anachekwa na kuonwa kuwa ni wa ajabu hali inayochangia vijana kujiingiza kwa kuhofiwa kuchekwa,” alisema Askofu Amani.
Mhashamu Amani aliwataka vijana kuachana na utandawazi, badala yake wafanye mambo yenye hekima na ya kuheshimika ili kuenzi utamaduni wa Kiafrika na kutii sheria za nchi.
Alisema vijana wakifuata sheria watakuwa watu wa haki, na kwamba watajitambua kiroho na kiakili hali itakayowafanya kuwa na nidhamu ya hali ya juu, ambayo itakuwa inapendeza jamii. Aidha, aliitaka Serikali, wazazi na walimu kukemea mambo hayo, ili Taifa liondokane na hali ya vijana kujiingiza katika mambo mabaya.
“Kutokana na utandawazi huo umekuwa ukiyumbisha vijana hali inayochanguia hata vijana wa vyuo vikuu kumaliza wakiwa wanatumia dawa za kulevya na Taifa kukosa kukosa watu wenye nguvu ya ”alisema .
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Charles Lekule, alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo, gari la wanafunzi, jengo la maabara ya sayansi pamoja na vifaa vya kujifunzia.
Alisema changamoto kubwa ni ubovu wa miundombinu ya barabara ya Kilemapofo, ambayo haipitiki licha ya kuwapo na taasisi nyingi za elimu za serikali, watu binafsi , na hospitali.
Source: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment