2014-10-24

MAREKANI WASHANGAZWA NA STORI ZA T.I KUHUSU TANZANIA, AKANUSHA KUWEPO KWA EBOLA


STAA wa Hip Hop kutoka nchini Marekani T.I Jumamosi iliyopita alipafomu kwenye tamasha la serengeti fiesta kinondoni, leaders club, ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuachia album yake iitwayo ‘’paper work’’, na ilikuwa ni katika kipindi ambacho Wamarekani wengi walikuwa wanaamini Afrika nzima inakabiliwa na gonjwa la Ebola.


Baada ya kurudi Marekani msanii huyo amekuwa akiulizwa mara nyingi kuhusu ishu hiyo ya Ebola na yeye amekuwa balozi mzuri wa Tanzania kwa kukanusha uvumi ambao huenda ulikuwa unatupunguzia fedha za kigeni, kupitia sekta ya utalii.

T.I pia ameshangazwa na umati wa zaidi ya watu elfu 50 kujitokeza kwenye serengeti fiesta pale leaders, na kusema namnukuu “tangu nianze kazi yangu hii sijawahi kuimba mbele ya umati wa watu zaidi ya elfu 50 tena wakiwa ni wenye asili ya africa” (weusi).

T.I amefunguka hayo kupitia kipindi cha Breakfast Show, na watangazaji wa kipindi hiko walishangazwa na idadi ya watu waliojitokeza kwenye Serengeti Fiesta, wakamuuliza je ulienda Tanzania wiki moja mbili au tatu kabla ili kupromote show, T.I akajibu no niliingia Tanzania siku hiyo hiyo na usiku wake kikanuka ile mbaya.


CloudsFM 

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...