2014-12-12

AFRIKA MASHARIKI IMENUFAIKA NA EALLYWOOD KWA WASANII

Baadhi ya wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki wanaounda EALLYWOOD wakiwa na Mratibu wao (aliyekaa katikati yao).
Msanii Slim na Hashim Kambi kutoka Tanzania pamoja na Margareth wa Kenya wakiwa katika mkutano.


Msanii Jackline Pentzel, Quincy kutoka Kenya na Fidelite wa Rwanda wakiwa katika pozi.

Mratibu wa EALLYWOOD akizungumza jambo na wanahabari (Hawapo pichani).

Msanii Quincy kutoka Kenya akisisitiza jambo.

Msanii Jackline Pentzel akijiandaa kuzumgumza na wanahabari (hawapo pichani).


KUFUATIA madai ya kunyonywa kwa wasanii kwa kufanya kazi kubwa katika jamii na kuwa na majina makubwa yasiyoendana na kipato chao, ikiwemo umaskini mkubwa walionao hatimaye baadhi yao wameamua kuanzisha East Africa Movie Club ‘EALLYWOOD’.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mratibu wa EALLYWOOD, Sanctus Mtsimbe ‘Spider Man’ alisema klabu hiyo ilianzishwa mwaka mmoja uliopita na ina jumla ya wasanii zaidi ya thelathini kutoka nchi za Afrika Mashariki, akiwemo Fidelite Sonia wa Rwanda, Quincy na Margareth (Kenya) huku Tanzania ikiwakilishwa na Jackline Pentzel, Rose Ndauka, Monalisa, Slim, Natasha, Tito, Hashimu Kambi, Haji Adam na wengineo.

Aidha msanii mkongwe kutoka Tanzania, Hashimu Kambi alisema kila nchi ina wanachama zaidi ya watano wa EALLYWOOD na kesho watawakaribisha wadau katika uzinduzi wa moja ya filamu ya ‘KAMATA FURSA’ iliyofanywa na wasanii hao.

Aliongeza kuwa filamu hiyo ni ya kimapinduzi na itazinduliwa kesho saa 1 jioni katika Hotel ya Akemi iliyopo Golden Jubilee, jijini Dar es Salaam.

GPL

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...