Pages

2014-12-09

Malaria: vifo vya pungua kwa 50%


               Ni picha ya mbu anayeeneza malaria.
Malaria imesababisha vifo hasa kwa Watoto wa chini ya umri wa miaka mitano .

Jitihada za kupambana na malaria zimefanikiwa kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo kwa kiasi cha asilimia hamsini.Shirika la afya duniani WHO limeeleza.

Shirika hilo limesema kati ya mwaka 2001 na 2013, idadi ya Watu milioni 4.3 walinusurika na ugonjwa huo katika nchi za chini ya jangwa la sahara, miongoni mwao milioni 3.9 ni watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.
                              


Kila mwaka , watu wengi zaidi wamepatiwa dawa za kuzuia na kupambana na ugonjwa huo.

Mwaka 2004 asilimia tatu ya watu walio hatarini kupata ugonjwa wa Malaria wamepatiwa neti , lakini sasa asilimia 50 ya watu wanapata huduma hiyo.

Mwaka 2013, nchi mbili, Azerbaijan na Sri Lanka, ziliripoti kuumaliza ugonjwa kwa mara ya kwanza , na nchi nyingine 11 (Argentina,Armenia,Egypt,Georgia, Iraq,Kyrgyzstan,Morocco,Oman,Paraguay,Turkmenistan na Uzbekistan) zilifanikiwa kupambana na kutokomeza ugonjwa huo.
                     


Asilimia 90 ya vifo vyote vya malaria hutokea barani Afrika, lakini sasa vifo hivyo vimepungua kwa kiasi kikubwa.

Idadi ya watu walioathirika na malaria imepungua kwa kiasi cha robo kutoka watu milioni 173 mwaka 2000 hadi milioni 128 mwaka 2013, ingawa kulikuwa na ongezeko la asilimia 43 barani Afrika katika maeneo yenye maambukizi ya ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment