Marekani imeionya Tanzania kuwa ufadhili zaidi kwa taifa hilo la mashariki mwa Afrika utategemea mafaniko ya jinsi inavyopambana na ufisadi.
Kulingana na shirika la kupambana na ufisadi duniani Transparency International,Tanzania imeshuka nafasi 17 katika orodha ya nchi fisadi duniani hadi nafasi 119,katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
Katika taarifa aliyoitoa hapo jana, balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress amesema hatua zinazopigwa nchini humo kukabiliana na ufisaidi ni muhimu katika kuamua kuendelea kwa nchi yake kuisaidia Tanzania, chini ya mpango wa ushirikiano wa kukabiliana na changamoto za Milennia MCC.
Bunge la Tanzania mwezi uliopita lilipiga kura kutaka baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu serikalini kuachishwa kazi, akiwemo mwanasheria mkuu,waziri wa nishati na mawaziri kadhaa kufuatia ripoti inayoonyesha kuna ufisadi mkubwa katika sekta ya nishati na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete anatarajiwa wiki ijayo kutoa uamuzi iwapo atawaachisha kazi maafisa hao.
0 comments:
Post a Comment