2014-12-24

Roho Juu; Sakata la Escrow

RAIS KIKWETE AKIONGELEA WANAOWASEMA VIBAYA KARUME NA NYERERE

24 Disemba 2014 Imebadilishwa mwisho saa 05:45 GMT Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete 


Nchini Tanzania mtikisiko wa matokeo ya kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow umeendelea baada ya Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi kusimamishwa kazi
 ili kupisha uchunguzi dhidi yake. Maswi anakuwa kiongozi wa tatu wa ngazi ya juu kukumbwa na upepo huo akitanguliwa na Mwanasheria mkuu wa serikali ambaye alijiuzulu mwenyewe 
 
na Waziri wa Ardhi aliyetimuliwa kazi hadharani na Rais Jakaya Kikwete. Licha ya kuondoka kwa viongozi hao bado baadhi ya wananchi na vyama vya upinzani wameendelea kulalamika kuwa juhudi za kutekeleza maazimio ya Bunge ni ndogo. Kuhusiana na hilo Baruan Muhuza wa BBC alizungumza na Neville Meena, katibu wa Jukwaa la wahariri Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...