2015-02-10

Chadema sasa kushambulia kwa kutumia mabaraza yake,,,je, wajua ni kwa nini bofya hapa kujua chanzo..........!!!!!!!!!!



Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeamua kutumia mabaraza yake kufanya mashambulizi ya kisiasa kujiimarisha miongoni mwa makundi maalum katika jamii.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka ndani ya chama hicho, chama hicho sasa kitayatumia mabaraza yake ya Vijana (Bavicha), Wanawake (Bawacha) na (Bazecha) kama mkakati wa kulenga makundi mahsusi ya wapiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Habari hizo zilisema kuwa chama hicho kiliyaagiza mabaraza hayo tangu mwaka jana kuhakikisha yanahamasisha makundi maalum katika jamii na kuwa mstari wa mbele kwenye mapambano ya kisiasa ya chama hicho.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...