2015-02-25

Mchakato wa kuimulika Mamlaka ya Bandari uwe endelevu



wezi Agosti mwaka 2012, aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alibadili ghafla mwelekeo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuwasimamisha viongozi wote waandamizi.

Dk Mwakyembe aliyejijengea heshima kubwa ya uadilifu katika Serikali aliwasimamisha aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Ephraim Mgawe na Naibu Mkurugenzi Mkuu Hamad Koshuma. Pa Naibu mkurugenzi Mkuu (miundombinu) Julius Mfuko na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Kasian Ngamilo.

Kusimamishwa kwa watendaji hawa na wengine kadhaa waliokuwa wakifanya kazi kwa ukaribu na uongozi wa juu, kulitokana na matokeo ya tume iliyoundwa na Waziri Mwakyembe kuthibitisha tuhuma kadhaa, ikiwamo uzembe uliokithiri, ufanisi duni na matumizi mabaya ya madaraka.

Kusimamishwa kwa watendaji hawa kulienda sambamba na kuteuliwa watendaji wapya kwa ajili ya kukaimu nafasi hizo ambapo mhandisi Madeni Juma Kipande alipata bahati ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka.

Kuteuliwa kwa Mhandisi Kipande kulipokelewa kwa shauku kubwa na wafanyakazi na hata Watanzania kwa kuamini kuwa atasaidia kuendeleza juhudi za Mwakyembe za kuisafisha taasisi hiyo na kuirejeshea heshima iliyokuwa imepoteza.

Hata hivyo, miaka kadhaa tangu yafanywe mabadiliko hayo, hali bado si shwari ndani ya mamlaka hiyo.Yapo malalamiko ya chini kwa chini kuhusu kuwepo kwa dosari za kiutawala kwenye, hali hali inayotishia kudorora kwa ukusanyaji wa mapato ya serikali .

Miongoni mwa malalamiko yanayotolewa na wafanyakazi yanashabihiana na yale yaliyoibuliwa na tume iliyoundwa na Dk Mwakyembe iliyosababisha kutimuliwa kwa watendaji waandamizi.

Hii si dalili njema kwa ukuaji wa uchumi wa taifa unaotegemea kwa kiasi kikubwa utendaji wa chombo hiki nyeti cha Serikali katika mapato.

Kukosekana kwa mshikamano na maelewano kati ya wafanyakazi na viongozi ni hatari kwa ufanisi wa taasisi.

Hakuna ubishi kuwa bandari ya Dar es Salaam ni miongoni mwa idara muhimu za Serikali zenye mchango mkubwa katika makusanyo ya mapato kwa Taifa.Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 43 ya makusanyo yote ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yanatokana na kodi na ushuru wa forodha ambayo miongoni mwake asilimia 87 yanakusanywa kupitia bandari hiyo.

Tayari Waziri wa Uchukuzi aliyeteuliwa hivi karibuni, Samwel Sitta ameingilia kati na kumsimamisha kazi kaimu mkurugenzi aliyekuwa akilalamikiwa. Naupongeza uamuzi wa Waziri Sitta wa kuwa msikivu na 
kuchukua hatua. Nakubaliana pia na uamuzi wake wa kuunda tume ya watu sita ya kuchunguza tuhuma za kiongozi huyo, lakini nachelea kuwa muda wa wiki mbili alioupa tume unatosha kukamilisha uchunguzi na kuja na majibu stahiki

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...