




PIKIPIKI iliyokuwa ikitokea Kimara imegongana na daladala aina ya DCM inayofanya safari zake kati ya Mbagala - Ubungo mchana huu eneo la Ubungo Mataa jijini Dar es Salaam.
Ajali hiyo imetokea wakati pikipiki na DCM vikivuka mataa hayo ambapo pikipiki imeingia uvunguni mwa DCM na kukokotwa huku ikitoa cheche zilizopelekea moto kuwaka na pikipiki hiyo kuteketea kwa moto. Aidha sehemu ndogo ya daladala hilo nayo ilishika moto wakati pikipiki ikiteketea.
Imeelezwa kuwa dereva wa pikipiki hiyo ameumia sana na hali yake ni mbaya kutokana na majeraha aliyoyapata.
0 comments:
Post a Comment