MOTO mkubwa ambao chanzo chake kinatajwa kuwa ni hitirafu ya umeme umeteketeza bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Idodi wilaya ya Iringa mkoani Iringa .
Tukio hilo limetokea muda wa saa 4 jana asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Kamanda wa jeshi la Zimamoto Mkoani Iringa, Inspekta Kennedy Komba alisema kuwa bweni hilo limeteketea lote na kuunguza mali zilizokuwamo kwenye bweni hilo na chache kuokolewa na wananchi waliowahi kufika eneo la tukio kusaidia kuzima moto huo.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo imesababishwa na hitalafu ya umeme na hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa na moto huo.
Tukio hilo kubwa kulikumba jimbo la Isimani linaloongozwa na mbunge wake Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa nyumba na ardhi.
Wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi Iringa wakishiriki kuzima moto katika bweni la wanafunzi wa kike shuleni hapo amnbalo lilikuwa likiwaka moto jana asubuhi.
0 comments:
Post a Comment