2015-02-11

Zaidi ya watu 200 wahofiwa kufariki kwenye ajali ya boti


Hii ni ajali kubwa ya kwanza kutokea kwa mwaka 2015 ikihusisha vyombo vya majini kupata ajali na kuua watu wengi ambapo zaidi ya wahamiaji 200 wamefariki baada boti mbili walizokuwa wakisafiria kuzama katika bahari ya Mediterrania walipokuwa wakijaribu kuzamia kwenda Ulaya.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema ni watu nane pekee ndio waliweza kuokolewa baada ya kukaa majini kwa siku nne huku wengine 203 kutojulikana waliko. 

Msemaji wa UNHCR Italia, Bi. Carlotta Sami aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa boti mbili zilihusika katika ajali hiyo na zilikuwa zikitokea Libya huku kila moja ikiwa na zaidi ya watu 100.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...