BAADA ya kuzagaa taarifa za staa wa filamu nchini Aunt Ezekiel kujifungua, mwanahabari wetu ametia timu nyumbani kwa Aunt na kujiridhisha pasipo na shaka kuwa mrembo huyo bado yu mjamzito na taarifa za kujifungua si za kweli.

Mitandao mbalimbali ya kijamii imeripoti taarifa za Aunt kujifungua kuanzia jana huku mingine ikimpongeza na kuweka kipande cha video kinachomuonyesha mwigizaji huyo akiwa ammbeba mtoto mchanga.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Aunt Ezekiel jana aliweka kipande cha video akiwa amembeba mtoto mchanga bila kuandika chochote.

0 comments:
Post a Comment