MWENYEKITI wa Chama cha Mabadiliko na Uwazi (ACT-Tanzania), Kadawi Limbu, amemtaka mwanachama mpya wa chama hicho Zitto Kabwe, kuachana na mawazo ya kugombea nafasi ya uongozi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu hadi atakapotimiza miezi sita ya uwanachama wake.
Limbu ambaye anapinga kuondolewa kwenye nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
¡°Mimi bado ndio mwanyekiti wa ACT- Tanzania kwa vile barua inayodaiwakuniondoa katika nafasi ya uenyekiti haikuwa halali na ili nifanya kupeleka suala hilo mahakamani kwa ajili ya kupata muongozo,¡±alisema Limbu.
Limbu, alisema hivyo kwa vile katiba ya chama hicho inaelekeza wazi kwamba mwanachama yeyote anayetaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi ni lazima uwanachama wake uwe umetimiza zaidi ya miezi sita tangu ajiunge na chama hicho.
¡°Mkiangalia mtaona Zitto ambaye amejiunga na chama hicho hivi karibuni katika mazingira tata, katiba haimruhusu kugombea nafasi yeyote katika chama chetu ni muombe kwamba andelee kuwa mwanachama wakawaida tu,¡±alisema Limbu.
Hata hivyo, mwenyekiti huyo, alimtaka Katibu Mkuu wa Chama hicho Samson Mwigamba kuacha kuwapotosha wanachamakuhusu uchaguzi huo kwani uchaguzi huo siyo halali kutokana na mwenyekiti huyo kwena mahakamai kupinga kuondolewa katika nafasi hiyo.
Akizungumzia chanzo cha mgogoro huo, Limbu alisema yote hayo yamechangiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutokana naofisi hiyo kufanya kazi kwa utashi huku ikitoa taarifa zinazochanganya katika vyama.
Aliwataka wanachama wa chama hicho kutambua kuwa msajili huyo siyo anayepanga uongozi ndani ya vyama vya siasa.
Limbu alidai kuwa ameamua kumpeleka Msajili katika Ofisi za Taasi ya Kuuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai kuwa amekula njama katika kumpa barua ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Limbu alitoa angalizo kwamba atapigana hadi kufa kuliko kuona chama hicho walichokianzisha kwa gharama kubwa kukiona kikiangukia mikononi mwa mafisadi.
Alisema kuna watu wanajiita wazalendo lakini ukiwafuatilia utabaini kuwa wamejivika kofia hiyo kwa ajili ya kunyang¡¯anya haki za haki za watu, watu hao ni sawa na majambazi.
Msemaji wa ACT-Tanzania, Abdallah Khamis, alisema katiba ya chama hicho, iliyoko kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, inaonesha kwamba mwanachama yeyote anaweza kugombea nafasi yeyote ya uongozi endapo ametimiza siku saba tangu ajiunge na chama hicho.
Pia alisema kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa kwa vile chama hicho hakina mgogoro wa kiuongozi mahakamani bali wanachojua shauri lililoko mahakamani ni la mtu binafsi.
¡°Huyu sio mwenyekiti tena wa chama chetu naomba muelewe hivyo amejiita mwenyekiti atakuwa amefanya makosa na kuna hatari ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria kuweni makini naye,¡±alisema Khamis.
Khamis, alimuonya aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa chama hicho kuacha kupitapita mitaani na kuwapotosha wanachama badala yake kama anataka kuwa kiongozi ajipange kugombea na yeyote katika uchaguzi huo Mach 28 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment