Wakati msanii wa Bongo Fleva,Snura Mushi yuko kimya kwa zaidi ya miezi kwa karibu miezi mitano na zaidi ili kupisha ujauzito wake ukue kwa siri hadi akajifungua mtoto wake wa tatu zaidi ya mwezi mmoja uliopita, Snura ijumaa iliyopita aliachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Hawashi’ na kuifichua siri yake ya kubeba ujauzito na kuficha siri hadi anajifungua.
Kwa mujibu wa meneja wa msanii huyo aitwaye Hk Hyper,alisema kuwa kipindi hicho wakati Snura akiwa mjamzito alikuwa akipigiwa simu mbalimbali za kufanya shoo na kwamba wamekosa pesa nyingi sana.

No comments:
Post a Comment