Huyo ni sajenti Simoni ambaye ni kachero anayedaiwa kuwa ni mtaalam wa kufungua Shampen akifanya makeke mbele ya kadamnasi kama anavyoonekana ili shughuli ya vinywaji iweze kuendelea
SHEREHE maalum ilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Ukonga kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 sambamba na kumuaga aliyekuwa kachero mkuu wa wilaya ya Kipolisi ya Ukonga ASP Idd Kyomo ambaye sasa anaenda Tabora.
Wilaya ya Ukonga inasifika kwa kuzalisha viongozi wa jeshi la polisi walio bora na hivi sasa wilaya hiyo inaongozwa na kamanda SP Jilio Simba ambapo aliandaa sherehe hiyo ya kukumbukwa.
0 comments:
Post a Comment