





j
U UWanafunzi wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang nchini China wameanzisha umoja wao na Jumamosi iliyopita wameuzindua rasmi umoja huo wenye lengo la kuwasaidia kwa mambo mbali mbali
wakiwa kwenye nchi ya kigeni.Jumla ya wanafunzi 54 wa Kitanzania wapo kwenye mjii huo wakiwa wanasoma kwenye vyuo mbali mbali na walikuwa hawana kitu chochote kinachowaweka karibu kama Watanzania na ndio maana wakaanzisha umoja huo.
Umoja huo unaojulikana kwa jina la Nanchang, Tanzanian Students Association (NATASA) ulizinduliwa rasmi na mwenyekiti wake Given Massawe ambae alisema kuanzishwa kwa umoja huo lilikuwa ni wazo la muda mrefu na hatimae hivi sasa ndoto imetimia.
Massawe alifafanua kuwa kwenye mingine ya nchini China ambako kuna wanafunzi wa Kitanzania nao wanajumuia zao ambazo zinawasaidia hivyo kwa wanafunzi wa Nanchang kuwa na umoja huo ni sehemu ya fungua milango kwao.
Massawe alifafanua kuwa kwenye mingine ya nchini China ambako kuna wanafunzi wa Kitanzania nao wanajumuia zao ambazo zinawasaidia hivyo kwa wanafunzi wa Nanchang kuwa na umoja huo ni sehemu ya fungua milango kwao.
Mwenyekiti huyo amesema hivi sasa wapo kwenye harakati za kutengeneza katiba yao ambayo ndio itakuwa dira ya uongozi wao na pia kuzinduliwa kwa chama hicho ni msaada tosha kwa wanafunzi hao wa Kitanzania kuanzia kwenye masomo hadi maisha ya kila siku.Uzinduzi wa umoja huo ulienda sambamba za sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania bara na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa Nanchang kusherekea siku yao ya Uhuru wakiwa pamoja. Michuzi
0 comments:
Post a Comment