Umoja wa Mataifa umeomba kiasi cha dola bilioni 16 kwa ajili ya shughuli za kibinadamu mnamo mwaka ujao wa 2015, ukisema idadi ya watu walioathiriwa na mizozo pamoja na majanga ya kimaumbile imefikia kiwango ambacho hakijawahi kuwepo kabla.
Takribani asilimia 40 ya fedha hizo zinatarajiwa kuushughulikia mgogoro wa Syria.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu Valerie Amos amesema watu wasiopungua milioni 78 wanahitaji msaada wa kibinadamu, na mipango ya umoja huo ni kuwapatia msaada wapatao milioni 57 miongoni mwa hao.
Nchi nyingine ambazo zimetiliwa maanani katika ombi la msaada huo ni Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini pamoja na Iraq. Bi Amos amesema fungu la fedha lililoombwa halihusishi nchi tisa za Ukanda wa Sahel pamoja na Djibouti, akiongeza kuwa ombi la msaada kwa ajili ya nchi hizo litatangazwa baadaye.
0 comments:
Post a Comment