Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limetangaza kwamba mwaka 2014 ulikuwa mwaka mbaya kabisa kwa watoto.
Kwa mujibu wa shirika hilo, watoto wapatao milioni 15 wameathiriwa na migogoro inayoendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati, Iraq, Sudan Kusini, Syria, Ukraine na Palestina.
Mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake ameeleza kuwa taarifa kuhusu adha wanazozipata watoto mara nyingi hazisikiki kutokana na migogoro mingine ya kimataifa inayogonga vichwa vya habari.
Lake amekumbusha kwamba watoto wasio na hatia wanauliwa wanapokuwa katika shughuli za kila siku kama vile wakiwa darasani au wakiwa wamelala.
Wengine wanateswa, kubakwa au kuchukuliwa mateka. Karibu watoto milioni 230 wanaishi katika nchi zilizoathiriwa na vita ulimwenguni kote
0 comments:
Post a Comment