Makubwa! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke wa mtu aliyekuwa akiishi ukweni na mumewe wa ndoa, Bahati Ramadhani, amenusurika kuuawa na ndugu wa mumewe wakiwemo mawifi na wakwe zake baada ya kudaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko wake na kujikuta wakigombea mtoto.
Tukio hilo la kushangaza lililojaza kadamnasi lilijiri nyumbani kwa wakwe hao, Mtaa wa Mawenzi jirani na Soko la Matunda la Mawenzi la mjini hapa wiki iliyopita ambapo Bahati alikuwa akiishi na mumewe, ldd Yusuf.
Ilielezwa kwamba wanandoa hao walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume (jina kapuni) ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 2.
0 comments:
Post a Comment