Dk Harrison Mwakyembe
Ni baada ya kuhamishwa kutoka Wizara ya Uchukuzi na kupelekwa Afrika Mashariki.
Dar es Salaam. Wasomi na wananchi kadhaa jana walizungumzia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete, wengi wakihoji sababu za kumhamisha Dk Harrison Mwakyembe kutoka Wizara ya Uchukuzi kwenda Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Rais alifanya mabadiliko kwenye baraza hilo baada ya mawaziri wawili kuanguka kutokana na kashfa ya uchotwaji takriban Sh306 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.
Ikiwa imesalia miezi isiyozidi sita kabla ya Baraza la Mawaziri kuvunjwa na akitakiwa kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Sospeter Muhongo, aliyekuwa Wizara ya Nishati na Madini na Profesa Anna Tibaijuka aliyekuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rais Kikwete alifanya mabadiliko 13, yakihusisha mawaziri wanane na manaibu watano.

Miongoni mwa mabadiliko hayo manane ya mawaziri, ni uhamisho wa Dk Mwakyembe kutoka Uchukuzi kwenda Afrika Mashariki huku Samuel Sitta, ambaye aliwahi kumwelezea mbunge huyo wa Kyela kuwa ni mmoja wa “marafiki wa kweli”, akihama kutoka Wizara ya Afrika Mashariki kwenda Uchukuzi.
Watu wengi walioongea na gazeti hili, walisema hakukuwa na haja ya kumhamisha Dk Mwakyembe kutokana na kazi nzuri ambayo ameshaifanya kwenye wizara hiyo, ambayo ina tatizo kubwa la usafiri wa reli, kuyumba kwa Shirika la Ndege (ATCL) na utendaji mbovu kwenye bandari, mambo ambayo Dk Mwakyembe alionekana kuyashughulikia kwa nguvu zote.
Sitta, mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, pia aliwahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).
“Tulikuwa tunaziona jitihada za Dk Mwakyembe,” alisema mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Frank Tily. “Na kuhamishwa kwake kunamaanisha kuwa mambo yote yaliyokuwa yanaendelea yatatakiwa kuanza upya. Nashindwa kuelewa ni kwa nini waziri huyu amebadilishwa… ingekuwa bora zaidi kama angeachwa.”
Dk Frank Tily alisema kuwa kutokana na haja ya kuongeza mawaziri ili kuziba nafasi mbili zilizoachwa wazi, hakukuwa na haja ya kuwabadilisha wale waliofanya vizuri katika wizara zao.
Aliongeza kuwa nafasi ya uwaziri isiwe inajazwa bila ya sababu za msingi, bali ifanywe tu endapo kuna haja kweli ya kufanya mabadiliko na akasisitiza kuwa “wizara ya uchukuzi haikuwa na sababu za kubadilishiwa waziri.”
Naye mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, Samwel Chacha alisema kuwa, mabadiliko hayo yatakuwa na athari japo zinaweza zisionekane kwa muda mfupi.
“Mwakyembe alikuwa na mipango ambayo ilianza kuonekana na kudhihirisha uzalendo katika Wizara ya Uchukuzi. Kama angeachwa aendelee nayo, kungekuwa na mabadiliko ambayo yangetutambulisha Watanzania kwa kuwa na vitu vyetu kwa manufaa ya nchi nzima,” alisema Chacha.
Ofisa Mikopo wa Benki ya NMB, Tito Mwanjala alisema mabadiliko yaliyofanywa, yamekosa mwonekano mpya kutokana na wabunge wengi kukosa sifa zinazotumika kuwapata mawaziri hao.
Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment