Zanzibar. Mshauri wa Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein katika masuala ya Utalii, Issa Ahmed Othman amefariki dunia akiwa katika matibabu nchini India.
Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed alisema Serikali tayari imeanza kufanya taratibu za kuurejesha mwili wa marehemu nyumbani.
Alisema mwili huo unatarajiwa kuwasili kesho na taratibu za mazishi na ratiba itatangazwa baada ya Serikali kupata mwongozo kutoka kwa wanafamilia.
“Ratiba ya mazishi itatangazwa baada ya wanafamilia kupanga na kutoa mwongozo...bado hatujafahamu kama atazikwa Pemba au Unguja,” alisema Waziri Aboud.
Alisema kwa sasa wanafamilia wanafanya vikao nyumbani kwa marehemu Mazizini, nje kidogo ya Manispaa ya Mji wa Zanzibar.
Wakati wa uhai wake, amewahi kuwa Naibu Waziri wa Kilimo chini ya Rais Idrisa Abdurlwakili, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwakilishi wa Jimbo la Pandani na mwenyekiti wa bodi mbalimbali za mashirika ya umma Zanzibar. Marehemu ambaye kitaaluma alikuwa mhasibu, aliongoza Kamisheni ya Utalii kwa muda mrefu kabla ya mwaka 2010 kuteuliwa kuwa mshauri wa mambo ya utalii.
Kutokana na utendaji wake sekta ya utalii Zanzibar imepata mafanikio makubwa na kuweza kuchangia aslimia 27 ya pato la Taifa na aslimia 83 ya fedha za kigeni.

0 comments:
Post a Comment