2015-02-02

KINAMAMA ‘UJIRANI MWEMA MBEZI’WALICHOKIFANYA NI MFANO KWA JAMII


Kinamama wakikabidhi zawadi kwa mlezi wa kituo.

Mwenyekiti wa kikundi, Rose Kanijo, akiongea na watoto hao.
Watoto wakipokea zawadi.

Mlezi wa watoto hao, Athumani Sultani, akitoa shukrani.

Mwenyekiti wa mtaa, Seif Salum, akitoa neno la shukurani.

Mmoja wa mama wa kikundi cha Ujirani Mwema akikata keki.
...Wakipata msosi.

Kinamama wa kikundi cha Ujirani Mwema Mbezi wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima.

KIKUNDI cha akina mama wa Ujirani Mwema Mbezi jana walitembelea kituo cha watoto yatima cha Alfurqan Islamic Centre kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam.

Kinamama hao wakiongozwa na mwenyekiti wao, Rose Kanijo, walitoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula, nguo na viatu vya watoto.

Mbali na msaada huo wanakikundi hao walipika chakula cha mchana na kujumuika na watoto wapatao hamsini ambao walikula nao. Pia walikata keki za baadhi ya watoto na wanachama waliokuwa wakiadhimisha siku zao za kuzaliwa.

Baada ya kisherehe hicho kidogo mlezi wa watoto hao, Athumani Sultani, alitoa shukrani zake kwa akina mama hao kwa kuwakumbuka watoto hao ambao wamekuwa wakihitaji misaada mbalimbali kutokana hali yao.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...