


Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka Mtaa wa Gerezani, Kariakoo jijini Dar es Salaam leo wamegoma kufungua maduka yao huku wengine wakiwa wamefungua maduka na kuendelea na biashara.
Wafanyabiashara hao wameamua kufunga maduka kwa kile kinachodaiwa kumuunga mkono Mwenyekiti wao, Johnson Minja (34), anayepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma kwa makosa mawili likiwamo la kuzuia ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki (EFDs).
0 comments:
Post a Comment