

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.
KAZI ya Yanga hivi sasa ni kama shoka! Kikosi hicho cha Kocha Hans van Der Pluijm kimeshinda michezo mitatu mfululizo kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuibugiza Tanzania Prisons mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa, jana.
Ushindi huo umeifanya Yanga ikwee kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikifikisha pointi 28, ikiwa imewafunika Azam FC kwa tofauti ya pointi mbili. Azam, jana ilibanwa mbavu na maafande wa Ruvu Shooting na kulazimishwa suluhu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORTS KWENDA NAMBA 15778

0 comments:
Post a Comment