2015-03-30

Abdul Bonge kuzikwa leo mkoani Morogoro

Mwanzilishi wa kundi la Tip Top Connection na Meneja wa kundi hilo, marehemu Abdul Shaban Tale Tale 'Abdu Bonge' anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao,Matombo mkoani Morogoro.

Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Kundi la Tip Top Connection na mdogo wa marehemu, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’, alisema siku ya tukio Abdul Bonge akiwa maskani ya Tip Top Connection iliyopo Magomeni-Kagera alifuatwa na kijana mmoja na kuambiwa rafiki yake aitwaye Nassoro Idd alikuwa akipigana na mkewe hivyo aliagizwa na mama yake Nassoro akamwite ili awasuluhishe.

Muda mfupi baada ya kwenda kwenye ugomvi huo zilirudi taarifa kuwa Abdul Bonge ameanguka na kupoteza fahamu.
Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo na kuwakabidhi mwili huo.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...