2015-03-07

MTUHUMIWA WA UBAKAJI ACHEZEA KIPIGO TAKATIFU NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI NA KUUAWA PAPO HAPO


Watu wakimshambulia mtuhumiwa wa ubakaji nchini India 

Maelfu ya watu walilivamia gereza moja kaskazini mashariki mwa India, na kumtoa kwa nguvu mtu mmoja aliyetuhumiwa kwa ubakaji na kisha wakamuua. 

Polisi imesema umati huo wa watu uliwazidi nguvu walinzi wa Gereza Kuu la Dimapur mjini Nagaland siku ya Alhamisi na kumkamata mshukiwa huyo wa ubakaji, ambaye pia walimtuhumu kuwa ni mhamiaji haramu kutoka Bangladesh. 


Askari mmoja amesema watu hao walimpiga na kumrushia mawe mpaka akafa. 
Polisi imesema amri ya kutotoka nje imewekwa katika mji huo baada ya mauaji hayo na kuwa hakuna visa vingine vya machafuko.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...