2015-03-10

NADIA BUHARI AJIFUNGUA MAPACHA WA KIKE MAREKANI...........bofya hapa kwa kumpa pongezi


Muigizaji wa Ghana Nadia Buhari amejifungua watoto mapacha wa kike nchini Marekani 

Taarifa kwamba muigizaji mrembo wa Ghana Nadia Buari amejifungua watoto mapacha wawili wa kike katika hospitali nje ya nchi zimesambaa Machi 2, 2015. 


Taarifa hizo zilithibitishwa na baba yake, Alhaji Sidiku Buari, wengi hawakuamini, huku wengine wakidai ni kama njia ya kutokea na kujitangaza. Hata hivyo, mrembo huyo alithibitisha taarifa hizo siku kadhaa zilizopita, akiwashukuru mashabiki wake kwa upendo wao. 



Nadia Buhari akiwa na Jim Iyke ambaye alikataa kuwa si baba wa mapacha hao 



Nadia alijifungua mapacha hao nchini Marekani. Hata hivyo, baba wa watoto hao bado hajajulikana. Tetesi zinazodai anaweza kuwa Jim Iyke zimekataliwa, huku muigizaji akijipanga kumtaja baba wa watoto wake warembo. 



Kulikuwa na taarifa hivi karibuni kwamba baba wa mapacha hao ni mtu fulani ambaye alisoma chuo kikuu pamoja naye huku ikidaiwa kuwa mahusiano na Jim Iyke yaliisha baada ya kuchumbiwa mwaka uliopita.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...