
Sintah kaamua kuvunja ukimya kuhusiana na 'Ubwege' wa Nuh Mziwanda ambaye anaripotiwa kuchapwa makofi, ngumi na mateke na mpenzi wake Shilole.
Nukuu ya hapo chini si maneno yetu, ni maneno ya mwanadada Sintah tuliyoyanukuu kama yalivyo toka kwenye blog yake
“Jamani jamani mnaosema ooh umasikini mmbaya kwanini Shilole anamdhalilisha bwana yake, jamani kwani huyo ‘so called’ Nuh or ‘whatever’ his name is kalazimishwa??
"Unajua siku hizi mapenzi yamemekuwa ‘free’ sana yaani ukiona mtu anakupa vitasa mara humuelewi yanini kun'ga'gania ‘as if’ umezaliwa naye?
"Mtu uliyemjua ukubwani nae akupe shida???... ‘BIG NO, i would rather stay single for the rest of my life’, kwanza sio adhabu kuwa ‘single’ kuliko kuwa katika ‘unhealthy relationship’ ...
"Mnaomuonea huruma huyo ‘so called’ Mziwanda ni wanafiki mapenzi.Kama anapigwa vitasa na anatulia anajua mwenyewe alichokifanya na atulie, kuliko kusema ni umasikini kwani yeye ni kiwete?
"Ina maana hawezi kutafuta kazi akapata mpaka awe msingi kiuno? ‘hell no’ muacheni apokee makonde, vitasa, nk.
"Vijana kama yeye wapo wengi tuu kazi ‘kujisexisha’ na kuwa msingi kiuno mjini ndio wanafanya taifa linadidimia kwa umasikini.
"Vijana wenye nguvu wanatakiwa wafanye kazi matokeo yake wanajipamba tu , halafu mnalalmika ooh wazee hawatuachii nafasi maofisini watawachiaje na nyie siku hizi mnapenda ‘slope, full kutelezaa…”
0 comments:
Post a Comment