2014-12-11

Ufisadi sasa ni janga, tuungane kuuangamiza kukomesha !!!!TUNAKUFUKULIA!!!!


Nani anabisha kuwa kuendelea kuichagua CCM ni kuendeleza majanga katika Taifa letu, kama yupo anayebisha basi huyo lazima dhamiri yake itakuwa imekufa.

Chama tawala CCM ni janga linaloendeleza umaskini katika kila sekta ya maisha ya Mtanzania; kielimu, kiafya, kiajira, kiuchumi, kiutamaduni, kifikra na hata kiimani.

Serikali ya CCM haiwezi kuondoa rushwa na ufisadi kwa sababu ni mtaji mzuri kwa uhai wake ili kuendelea kubaki madarakani. Bila matumizi ya rushwa na ufisadi hakiwezi kupita chaguzi kwa kishindo.

CCM kama chama tawala inatakiwa kuwa mfano mzuri wa kuendesha siasa kidemokrasia kwa, amani na usawa kwa vyama vingine nchini.

Kumbe kujigamba kwamba CCM inakubalika na wananchi si kweli, na ukweli ni kwamba inatumia mtaji wa ujinga na umaskini wa watu ili kuwarubuni wananchi ambao bado hawajitambui.

Mwalimu JK Nyerere kama nabii alitabiri mambo mengi sana ambayo mengi yametokea na mengine yanaendelea kutokea na yataendelea kutokea siku za usoni.

Mfano mzuri ni ule utabiri wake kuwa “Ikulu ni mahali patakatifu” mnakimbilia kufanya biashara gani huko? Hili limetokea na linaendelea kutokea na kuna hatihati hata hii skandali ya escrow imegusa Ikulu pia.

Nukuu nyingine ya Mwalimu Nyerere inayowafaa Watanzania waitafakari katika kipindi hiki cha ufisadi mkubwa ni hii:

“Serikali ya rushwa popote pale, haitozi kodi. Serikali ya rushwa inatumwa na wenye mali, inawafanyia kazi wenye mali. Serikali ya rushwa itamwambiaje mwenye mali, kwamba “utalipa, usipolipa utakiona” Atacheka tu huyu. Atakwambia “unaniambia hivyo wewe? Kesho siji basi.” Mwalimu alishaliona hili ndiyo maana aliliweka wazi kabisa kwa viongozi wa Serikali yetu.

Na leo tunashuhudia kwamba Serikali imelalamikiwa sana kuhusu ufisadi.

Lakini kitu kikubwa ambacho Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikisema na kimetokea ni kile cha Serikali ya wala rushwa haikusanyi kodi.

Sasa kwa mfano katika yale mabilioni ya escrow yaliyogawanywa katika maboksi, mifuko ya rambo na magunia, je, kodi ililipwa?


Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...