Dalili za mwanzo mbaya kwa Barca zilionekana tangu mapema baada ya beki wa kushoto Jordi Alba kujifunga mwenyewe kwa kichwa akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa toka upande wa kulia .
Bao hili lilidumu hadi mwisho wa mchezo huku Real Sociedad walio chini ya kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes wakikomaa na kuwazuia Barcelona katika shambulizi walilopanga .

Wachezaji wa Real Sociedad wakishangilia baada ya beki wa Barcelona kujifunga .Pamoja na ukweli kwamba wengi watashangazwa na matokeo haya , ukweli ni kwamba
takwimu hazikuwa na ishara nzuri kwa Barcelona kwani mabingwa hawa wa zamani wa ulaya hawajawahi kushinda mchezo wowote kwenye uwanja wa Real Sociedad Estadio Annoetta tangu mwaka 2008 ambapo katika michezo mitano iliyopita walifungwa mara nne huku wakitoka sare mara moja .
Kipigo hiki kimewanyima Barcelona fursa ya kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi ya Hispania baada ya kuwashuhudia wapinzani wao Madrid wakipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Valencia.

Kocha wa Sociedad David Moyes akiwa kwenye harakati za kuwaelekeza wachezaji wake kwenye mchezo dhidi ya Barcelona.

Benchi la Barcelona wakati wa mchezo dhidi ya Real Sociedad.Kwa matokeo haya Real Madrid wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 39 wakiwazidi kwa pointi moja wapinzani wao Barcelona wenye pointi 38 sawa na mabingwa watetezi Atletico Madrid japo vijana wa Carlo Ancelotti wana faida ya mchezo mmoja mkononi ambao endapo watashinda wataomgeza tofauti ya pointi baina yao na wapinzani wake wa karibu kwa pointi tatu zaidi.

Msimamo wa ligi ya Hispania kama ulivyo baada ya michezo ya wikiendi hi

0 comments:
Post a Comment