2015-02-16

Membe aiomba China iiokoe Tazara......je,wajua ni kwa nini fuatilia kisa hapa



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Ajiandaa kukutana na Rais wa Zambia kupanga mapendekezo ya nini kinapaswa kufanyika

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameiomba Serikali ya China kusaidia kuimarisha ufanisi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara). 

Membe alisema hayo juzi usiku katika Sherehe ya Mwaka Mpya wa China, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akihutubia mamia ya Wachina wanaoishi nchini na baadhi ya Watanzania waliohudhuria sherehe hizo, Membe alisema anafanya mpango wa kukutana na Rais wa Zambia na kuandaa mapendekezo watakayoyawasilisha kwa Serikali ya China.

Alisema reli ya Tazara ni eneo linalotumika kwa kiasi kikubwa kuunganisha mataifa hayo kiuchumia kwani Zambia haina bandari na hutumia reli hiyo kusafirisha bidhaa kutoka Dar es Salaam kwenda Zambia.

Akizungumzia uhusiano wa Tanzania na China, Membe alisema nchi hizo ni marafiki katika nyanja mbalimbali na anaamini kuwa uhusiano huo utadumishwa kwa maendeleo ya mataifa yote mawili. 


Katika sherehe hizo, vikundi mbalimbali vya utamaduni vya China vilitumbuiza kwa maonyesho ya sanaa.

Balozi wa China nchini, Lu Youqing alisifu ushirikiano wa Tanzania na nchi yake na kusema kuwa utaendelea kudumishwa na pande zote mbili. Aliwapongeza Watanzania kwa kuungana nao kusherehekea siku hiyo huku akisema hii ni mara ya sita kwa nchi yake kuadhimisha sherehe hiyo nchini.
Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...