
Mashoga
Wakereketwa wa haki za binadamu nchini Uganda wanawashutumu polisi wa nchi hiyo, kwa kuwanyanyasa na kuwapiga wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Kundi hilo liitwalo Chapter Four Uganda, linasema limeorodhesha visa kadhaa ambavyo polisi wanawalazimisha wanaume kuvua nguo zao na kubaki uchi, ili kuonyesha sehemu zao nyeti kubaini iwapo wanahusika katika matendo hayo ya ngono ya jinsia moja.
Waziri wa msawala ya ndani nchini Uganda Jenerali Aronda Nyakairima, ameiambia BBC kuwa madai hayo si ya kweli, lakini akasema kuwa afisi yake itayachunguza.
0 comments:
Post a Comment