
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (CCM) kwa mara nyingine amechomoza na kushika nafasi ya kwanza kwa kupata kura 752 sawa na asilimia 22.8 ya kura 3,298 katika nafasi ya kiongozi anayefaa kuwa rais wa Tanzania.
Lowassa amepata kura hizo katika ripoti ya utafiti uliopewa jina la Vigezo na Matarajio ya Wananchi katika Kufanya Maamuzi ya Kuchagua Viongozi Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
Utafiti huo umefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Tanga, Lindi, Dodoma, Mtwara, Pwani, Kilimanjaro, Morogoro, Mwanza, Shinyanga na Iringa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Rais wa Shirika lisilo la kiserikali la Wanafikra Chanya nchini (PTT), Tibatizibwa Yabutinga alisema utafiti huo ulihusisha mikoa 13 ya Tanzania Bara.
“Lowassa alipata kura hizo dhidi ya wenzake 14 ambao wengi kati yao ni wale waliotangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ifikapo Oktoba mwaka huu,” alisema.
Alisema Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa alifuatia kwa kura 644 sawa na asilimia 19.5, Mwigulu Nchemba (CCM) kura 350 asilimia 10.6, Ibrahimu Lipumba (CUF) 294 sawa na asilimia 8.9, John Magufuli (CCM) 227 sawa na asilimia 6.8, Zitto Kabwe (ACT-Tanzania) 224 asilimia 6.7.
Alisema Benard Membe (CCM) alipata kura 197 sawa na asilimia 5.9, Mizengo Pinda (CCM) kura 107 aslimia 3.2, Samuel Sitta (CCM) 72 aslimia (2.2), Januari Makamba (CCM) 54 aslimia 1.6, Mark Mwandosya (CCM) 40 asilimia 1.2.
Alisema James Mbatia (NCCR- Mageuzi) alipata kura 34 sawa na asilimia 1, Hussein Mwinyi (CCM) kura 31 sawa na asilimia 0.9, Steven Wassira (CCM) 31 asilimia 0.4 na Frederick Sumaye (CCM) kura 10 sawa na asilimia 0.3.
0 comments:
Post a Comment