
Meninah amekanusha uvumi uliozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muimbaji wa ‘Siachani Nawe’ Barakah Da Prince.
Akizungumza na Bongo5, Meninah amesema kuwa ni kweli amekuwa akionekana kuwa karibu na msanii huyo lakini ifahamike kinachowaweka karibu ni kazi yake ya muziki.
“Sitembei na Barakah, kwa sababu Barakah Da Prince ni kama mdogo wangu, najuana nae toka hajaanza muziki hata alivyoanza mimi nilikuwa support yake kubwa katika kumshauri hivi na hivi yani vitu vitu vichache katika muziki, so kuna project yetu na itatoka ya kwangu mimi na yeye kuna song ameniandikia ambayo tayari nimeshaifanya na ipo tayari, kukaa na mtu karibu siyo kwamba unatoka nae jamani, nilikuwa nae sana karibu , tulikuwa tuna studio session nilikuwa nampitia kwao lakini sio kwamba niko nae,” alimalizia Meninah.-->
0 comments:
Post a Comment