2015-01-29

HAYA SASA;BELLA AANGUKIA KWA SERENGETI BOY


Na Waandishi Wetu/Amani
SABABU za Bella kuachana na mpenzi wake Luten Karama, zimetajwa kuwa ni serengeti boy ambaye ni mwanamuziki anayejulikana kwa jina la Dogo Nasri. 


Isabela Mpanda, 'Bella' akiwa na serengeti boy, 'Dogo Nasri'.

Sosi wa habari hii alisema kuwa Bella amekuwa akitoka kimapenzi na ‘underground’ huyo na ndiyo maana amekubali kirahisi kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi.

“Ulishawahi kuona Bella anakubali kuachia ngazi kirahisi hivyo? Mwenzako amekamatika kwa dogo si mchezo, anaonekana naye viwanja kwani hata alipotamka maneno ya kuachana na Kalama mwenyewe hakuwepo alikuwa mkoani Lindi, sijui akirudi itakuwaje,” alisema sosi.

Bella akipozi kimahaba na serengeti boy huyo.

Baada ya kupata ubuyu huo, mmoja wa waandishi wetu alimpigia simu Bella na kumsomea ‘mashtaka’ yake ambapo alisema hakuwa tayari kuzungumzia mambo yake ya uhusiano kwa sasa.

“Jamani ni mapema mno, bado nina maumivu nisingependa kuongelea mapenzi tena,” alisema Bella.
Nasri alipoulizwa alishindwa kuweka wazi na kudai kuwa Bella ni rafiki yake wa karibu anayeshirikiana naye katika kazi.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...